Wapenzi wa jinsia moja wazuiwa kuhudhuria kikao cha UN

Haki miliki ya picha Getty
Image caption LGBT

Kundi moja la nchi 51 za kiislamu limeyazuia mashirika ya kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja kushiriki katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi mwezi ujao.

Misri,inayowakilisha mashirika ya Kiislamu ilimuandikia rais wa mkutano huo wakitaka makundi hayo kuzuiwa kushiriki.

Marekani,Muungano wa Ulaya na maafisa wa Canada wamemuamdikia rais wa shirika hilo lenye wanachama 193 wakipinga kushiriki kwa watu hao.

Wawakilishi wa Misri hawakutoa sababu wa kutaka makundi hayo kupigwa marufuku.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkutano wa UN

Balozi wa Marekani Samantha Power amesema kuwa makundi hayo yalionekana kuchaguliwa kwa kushiriki kwao katika harakati za wapenzi wa jinsia moja na watu wanaobadili jinsia.

''Huku ikiwa watu wanaobadili jinsia wana uwezekano mara 49 wa kuishi na virusi vya ukimwi ikilinganishwa na idadi ya watu wa kawaida,kuzuiliwa kwao katika mkutano mkubwa kama huo kutaathiri maendeleo katika vita dhidi ya ugonjwa huo'',alisema Bi Power katika barua aliyomwandikia rais wa mkutano huo Mogenns Lykketoft.