Msichana wa Chibok apatikana Nigeria

Image caption Zaidi ya wasichana 200 wa walitekwa nyara na Boko Haram zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Wanaharakati nchini Nigeria wanasema kuwa mmoja wa wasichana wa shule wa Chibok, waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram amepatikana, akiwa ndiye mtu wa kwanza kukolewa kwa zaidi ya miaka miwili.

Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram kutoka mji ulio Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kampeni za kutaka kuokolewa wasichana wa Chibok.

Mwanaharakati Hauwa Abdu aliiambia BBC kuwa, msichana huyo alipatikana siku ya Jumanne jioni na kundi moja la kuweka ulinzi baada ya makabiliano na watu wanaokisiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.

Kiongozi mmoja wa kijamii alisema kuwa msichana huyo alikuwa na mtoto na wote wamekabidhiwa jeshi la Nigeria katika mji wa Damboa.