Wakuu wa mashtaka wataka Bemba apewe hukumu ndefu

Haki miliki ya picha
Image caption Bemba alishindwa kuwazua waasi wake waliokuwa wakiwaua na kuwabaka watu katika taifa jirani la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Waendesha mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita wametaka aliyekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jean Pierre-Bemba, kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 25 jela baada ya kupatikana na hatia ya kushuriki kwenye uhalifu wa kivita mjini Hague.

Bemba mwenye umri wa miaka 53 alipatikana na hatia mwezi Machi, kwa kushindwa kuwazua waasi wake waliokuwa wakiwaua na kuwabaka watu katika taifa jirani la Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 na 2003.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hii ndiyo mara ya kwanza mahakama ya ICC imeliangazia suala la ubakaji kuwa silaha ya vita.

Alikuwa amewatuma zaidi ya wapiganaji 1000 kusaidia kuzima jaribio la mapinduzi.

Hii ndiyo mara ya kwanza mahakama ya ICC imeliangazia suala la ubakaji kuwa silaha ya vita, na mara ya kwanza mshukiwa amepatikana na hatia ya uhalifu uliofanywa na watu wengine waliokuwa chini ya uongozi wake.