Rais wa kampuni ya Mitsubishi kujiuzulu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Mitsubishi Tetsuro Aikawa kujiuzulu

Kampuni ya magari ya Mitsubishi imetangaza kuwa rais wake Tetsuro Aikawa atajiuzulu wakati ambapo kampuni hiyo inakabiliwa na kashfa ya udanganyifu wa vipimo vya mafuta kwa miongo kadhaa.

Baada ya hisa za kampuni hiyo kuanguka kwa zaidi ya asilimia 50,kampuni ya magari ya Nissan iliingilia kati ili kuchukua udhibiti fulani wa hisa.

Mnamo mwezi Aprili,Mitsubishi ilikiri kufanya udanganyifu wa vipimo vya mafuta kwa kipindi cha miaka 25 iliopita.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption kampuni ya magari ya Mitsubishi

Wakati huohuo kampuni nyengine ya kutengeza magari ya Suzuki pia imebaini matatizo katika vipimo vyake vya mafuta lakini ikakana kufanya udanganyifu wowote.

Kampuni hiyo imesema kuwa ukaguzi wake wa magari yake 16 haikuzingatia sheria rasmi za kampuni hiyo,lakini ikasisitiza kuwa vipimo vipya vimebaini kwamba haukana haja ya kuifanyia marekebisho data hiyo.