Onitsha ndio mji wenye hewa chafu zaidi duniani

Image caption Onitsha uliandikisha viwango vilivyo juu mara 30 zaidi ya viwango vya uchafuzi vilivyowekwa na WHO.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la afya duniani WHO, unaonyesha kuwa mji wa Onitsha nchini Nigeria una hewa iliyochafuka zaidi duniani.

Onitsha uliandikisha viwango vilivyo juu mara 30 zaidi ya viwango vya uchafuzi vilivyowekwa na WHO.

Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa miji mingine mitatua nchini Nigeria ikiwemo Kaduna,Umuahia na Aba pia inaonekana kwenye orodha ya miji ishirini yenye hewa chafu zaidi duniani.