Virusi vya Zika kuingia Ulaya

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Virusi vya Zika

Virusi vya ugonjwa wa zika vinaweza kusambaa na kuingia Ulaya wakati wa majira ya kiangazi ,ijapokuwa uwezekano wa mlipuko wake uko chini kwa wastani, kulingana na shirika la afya duniani.

Maeneo ambayo yamo hatarini ni yale ambayo mbu aina ya Aedes huenda wakasambaza virusi hivyo ,kama vile pwani ya bahari nyeusi huko Urusi,Georgia na kisiwa cha Madeira.

WHO linayataka mataifa kuyaondoa maeneo yanayozalisha mbu na maeneo yake na kuhakikisha kuwa watu hususan waja wazito wana habari kuhusu athari za ugonjwa huo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa afya wakikabiliana na virusi vya Zika

Shirika hilo linasema kuwa mataifa mengi ambayo huenda yakaathiriwa yamejiandaa kukabiliana na visa vipya na kukabiliana navyo kwa haraka,lakini mataifa mengine yatalazimika kukabiliana na ugonjwa huo.