Wanajeshi watano wa UN wauawa Mali

Image caption Umoja wa mataifa unajaribu kurejesha amani kaskazini mwa Mali

Walinda amani watano wa umoja wa mataifa wameuawa katika eneo lililo kaskazini mwa Mali la Kidal baada ya kuvamiwa.

Kikosi hicho cha wanajeshi kutoka Chad kwanza kilishambuliwa na kilipuzi siku ya Jumatano na kisha baadaye kufyatuliwa risasi kutoka kwa kundi lisilojulikana.

Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo.

Umoja wa mataifa unajaribu kurejesha amani kaskazini mwali, eneo ambalo lilidhibitiwa mwaka 2012 na wanamgambo kutoka kabila la Tuareg.