Rais Maduro kuongeza mamlaka

Image caption Rais Nicolas Maduro wa Venezuella

Rais wa Venezuella, Nicolas Maduro, amesema yuko tayari kuongeza mamlaka yake chini ya utawala wa hali ya hatari iliyotangazwa wiki iliyopita.

Hatua hiyo imefikiwa ili kukabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali ya taifa hilo. Maduro amedai kuwa upinzani unachochea ghasia na pia kupanga njama ya kuipindua serikali yake. Amesema hatasita kuchukua hatua zinazofaa ili kudumisha amani nchini Venezuela, ambayo inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi.