Kifaa cha kudhibiti matumizi ya fedha chazinduliwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kifaa hicho kitadhibti matumizi ya fedha kwa kuwapatia wateja mshtuko.

Kampuni mmoja ya uingereza inatarajia kuweka kifaa kinachodhibiti matumizi ya pesa kwa kuwapatia wateja wake mshtuko wa umeme iwapo watapitisha kiwango cha matumizi yao.

Kampuni ya Intelligent Environments,imezindua mfumo ambao utaiunganisha na mpiro wa kuvaliwa mkononi wa Pavlok ambao unatoa mshtuko wa volti 255 kwa akaunti ya benki,iwapo fedha katika akaunti zitashuka kupita kiwango mteja alichokubali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pia mpira huo una uwezo wa kufanyakazi na mita za umeme kuzia matumizi ya juu ya umeme.

Pia mpira huo una uwezo wa kufanyakazi na mita za umeme kuzia matumizi ya juu ya umeme na kuokoa bili iwapo fedha hizo zitashuka.

Mtendaji mkuu wa kampuni Intelligent Environments,David Webber ameiambia BBC Wazo hilo lilikuwa kuhusu mapendekezo ya wateja.

Hakuna benki yoyote imetangaza itaazisha mfumo huo kwa wateja wake lakini benki hiyo ya mtandao ya Intelligent Environments imetaja benki kadhaa za uingereza kama wateja wao ambao wanatumia mifumo yake ya mitandao.