Wanawake wanyanyuaji uzito wajitosa ulingoni

Image caption Antoinette Kriel

Wanawake wa Afrika Kusini wanaoinua uzito wameonyesha ukakamavu wao katika mchezo unaoaminika kuwa wa wanaume.

Uinuaji wa uzito umechukuliwa tangu jadi kuwa swala la wanaume, lakini hivi majuzi wanawake wengi wamejiunga na mchezo huo.

Wiki hii mashindano ya kimataifa ya Bench Press yatakuwa yanaandaliwa katika mji wa Potchefsroom nchini Afrika Kusini huku kila jinsia ikiwakilishwa.

Miongoni mwa wanawake ambao watashiriki ni Antoinette Kriel.