Nigeria: Jeshi lampata msichana wa 2 wa Chibok

Haki miliki ya picha Nigeria Army

Msichana wa pili kutoka kwa wale 200 waliopatikana katika mji wa Nigeria wa Chibok amepatikana,jeshi limesema.

Lakini msemaji wa wazazi wa wasichana hao wa Chibok ana wasiwasi kuhusu madai hayo akisema kuwa jina la msichana huyo haliko miongoni mwa wale waliopotea.

Msemaji wa Jeshi amesema kuwa Serah Luka ni miongoni mwa wanawake 97 na watoto waliookolewa na jeshi kaskakazini mashariki.

Kundi la wapiganaji wa Boko haram limewateka nyara maelfu ya wasichana wengine katika miaka ya hivi karibuni,kundi moja la kupigania haki limekadiria.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ramani ya eneo la Sambisa

Hatua hiyo inajiri siku mbili baada kuokolewa kwa msichana wa kwanza wa Chibok ,Amina Ali Nkeki.

Katika taarifa yake ya awali baada ya kupatikana kwa Bi Nkeki ,jeshi lilimtabulisha kwa jina jingine.

Hatahivyo ni wasichana 218 ambao hawajapatikana baada ya kutekwa nyara na Boko Haram kutoka kwa shule ya upili ya Chibok kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2014.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana wa Chibok

Bi Nkeki aliambia kiongozi wa jamii ya Chibok kwamba sita kati ya wasivhana waliotekwa nyara wamefariki,lakini wengine bado wako ndani ya msitu wa sambisa ambapo alipatikana.