Meya aahidi zawadi kwa wanaoua wahalifu

Osmena Haki miliki ya picha EPA
Image caption Osmena amesema hilo litawatia hofu watu wanaopanga kutekeleza uhalifu

Meya wa jiji moja nchini Ufilipino ameahidi zawadi kwa watu wanakaowaua au kuwaumiza wahalifu.

Tomas Osmena, aliyechaguliwa kuwa meya mpya wa jiji la Cebu, ameahidi kutoa zaidi ya dola 1,000 kwa kila mshukiwa anayeuawa.

Amesema lengo kuu ni kuzua hofu na wasiwasi miongoni mwa wahalifu.

Bw Osmena tayari amemzawadi polisi ambaye hakuwa kwenye zamu aliyewapiga risasi na kuwajeruhi washukiwa wawili wakati wa jaribio la wizi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw Duterte amependekeza wahalifu wawe wakiuawa

Mpango wa meya hiyo unakaribiana sana na msimamo wa Rais mteule Rodrigo Duterte ambaye ameahidi kutoa amri ya kuuawa kwa wahalifu kama njia ya kukabiliana na uhalifu.