Mji wa India wavunja rekodi ya vipimo vya joto

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Joto kali India

Mji mmoja katika jimbo la Rajasthan nchini India umevunja rekodi baada ya kusajili vipimo vya juu vya joto vya hadi 51 C,ikiwa ni vya juu tangu kuanzishwa kwa rekodi za viwango hivyo ,kulingana na ofisi ya hali ya hewa.

Rekodi hiyo mpya katika eneo la Phalodi katika jimbo hilo la jangwa inajiri wakati ambapo kuna wimbi la mvuke joto kali nchini India.

Rekodi ya awali ya vipimo vya juu vya joto ilikuwa 50.6C mnamo mwaka 1956.

Wimbi hilo la Joto hilo limekumba eneo kubwa la India Kaskazini ambapo joto limepita vipimo vya 40C kwa wiki kadhaa sasa.

Wakati wa msimu wa upepo nchini India huwa na jua kali na kupanda kwa vipimo vya joto ,lakini viwango vya joto vinavyopanda hadi 50C sio vya kawaida.

Murari Lal Thanvi,shahidi mmoja huko Phalodi amiambia BBC ,kwamba alijaribu kukaa nje siku ya Ijumaa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Joto kali India

''Hata simu yangu ilisalimu amri na kuwacha kufanya kazi nilipokuwa nikipiga picha'',alisema.

Nilifanikiwa kuiwasha simu yangu baada ya kuiweka kitambaa chenye maji kwa takriban dakika 20-25.