Saa ya Haile Selassie yarejeshewa ‘mmiliki’

Haki miliki ya picha Getty

Maafisa wa mahakama nchini Uswizi wameamua kukabidhi saa iliyotumiwa na Mfalme Haile Selassie kwa mtu aliyepatikana na saa hiyo, shirika la habari la Bloomberg limeripoti.

Familia ya Selassie ilisema saa hiyo iliibiwa kutoka kwenye Kasri la Mfalme na wanajeshi waliotekeleza mapinduzi ya serikali mwaka 1974 au ikaibiwa kutoka kwenye sefu muda mfupi baada ya mapinduzi.

Waendesha mashtaka mjini Geneva wanasema hawakupata ushahidi wowote kwamba aliyekuwa na saa hiyo aliipata kupitia njia ya uhalifu.

Haki miliki ya picha AP

Bloomberg wanasema saa hiyo ya muundo wa Patek Phillipe iliyopambwa kwa dhahabu inaweza kuuzwa £1m (£690,000) kwenye mnada.

Kampuni ya kupiga mnada ya Christie imekataa kufichua jina la mtu anayemiliki saa hiyo na ambaye anapanga kuiuza mnadani.