Kimbunga kikubwa chaikumba Bangladesh

Haki miliki ya picha focus bangla

Takriban watu watano wameuawa nchini Bangladesh na maelfu ya wengine kuachwa bila makao wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa kuwasili kwa kimbunga.

Upepo mkali na mvua kubwa viling'oa miti na baadhi ya nyumba kuporomoka huku bandari nyingi zikifungwa.

Maafisa wanasema kuwa wako kwenye shughuli ya kuwahamisha zaidi ya watu milioni mbili kutoka sehemu za nyanda za chini pwani mwa nchi hiyo.