Apigwa risasi kwa kubeba silaha nje ya Ikulu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ikulu ya White House

Afisa wa usalama wa Marekani amempiga risasi na kumjeruhi mwanamume mmoja aliyeonekana amebeba bunduki nje ya Ikulu ya White House.

Maafisa wa Usalama wamesema kuwa mtu huyo alielekea kwenye mojawapo wa milango ya kuingia katika Ikulu huku amebeba silaha hiyo. Alipoamriwa aiweke chini silaha hiyo chini akakaidi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Walinzi kwenye Ikulu ya White House

Watu walizuiliwa kukaribia Ikulu hiyo ya White House kwa muda, huku maafisa wa Usalama wakikimbia kuhakikisha kuwa Makamu wa Rais Joe Biden, aliyekuwa katika jengo hilo wakati huo, alikuwa salama.

Rais Obama alikuwa ameondoka kwenda kucheza mpira wa gofu.

Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa walisikia mlio wa risasi na kisha wakamwona mwanamume mmoja mzungu akianguka chini.