Ajeruhiwa vibaya baada ya kuingia hifadhi ya Simba

Haki miliki ya picha Linton Zoo
Image caption Mwanamme aruka makusudi kwenda kwa hifadhi ya simba Chile.

Simba wawili wameuawa na walinzi wa hifadhi ya wanyama nchini Chile wakati walijaribu kumuokoa mwanamme mmoja ambaye alivua nguo na kisha kuruka kwenda kwa hifadhi walimokuwa simba hao.

Mwanamme huyo wa umri wa miaka 20 alijeruhiwa vibaya baada ya kuingia kwenye hifadhi hiyo ya simba na kuanza kuwachokoza simba akitaka wamshambulie.

Walinzi wa hifadhi walijibu kwa kuwafyatulia risasi simba hao walipoanza kumshambulia na kuwaua wote wawili.