Mabondia wa Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Mabondia washinda mapigano yao Kenya

Mabondia watatu wa timu ya taifa ya Kenya, Nick Okoth, Elly Ajowi na Aziz Ali walishinda mapigano yao katika fainali ya mkondo wa pili wa ligi kuu ya ndondi ya Kenya mjini Kisumu, huku bingwa mtetezi Polisi wakiibuka mshindi kwa kuzoa pointi 20, wakifuatiwa na Jeshi na Magereza. Mabondia hao watatu ni miongoni mwa wanamasumbwi sita watakaoshiriki katika mashindano ya kufuzu kwa michezo ya Olympiki mjii Baku, Kazakstan mwezi ujao.