Iraq yatangaza vita vya kukomboa Fallujah

IS Haki miliki ya picha AFPGetty Images
Image caption Wapiganaji wa IS wamedhibiti mji wa Fallujah kwa miaka miwili

Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametangaza operesheni kubwa ya kijeshi ya kuukomboa mji wa Fallujah kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Kundi hilo liliuteka mji huo miaka miwili iliyopita.

Akiwa ameandamana na maafisa wakuu wa jeshi, Bw al-Abadi alitoa tangazo hilo moja kwa moja kupitia televisheni na kusema bendera ya Iraq karibuni itapepea katika mji wa Falluja.

Mji huo unapatikana takjriban kilomita 50 magharibi mwa mji wa Baghdad.

Haki miliki ya picha AFP

Wanajeshi na polisi zaidi wametumwa kuuzingira mji huo.

Maafisa wa serikali awali walikuwa wamewatahadharisha maelfu ya raia ambao bado wamo katika mji huo, wengi wao jamaa za wapiganaji wa IS, kuuhama mji huo.

Licha ya kukabiliwa vikali, wapiganaji wa IS bado hudhibiti maeneo makubwa kaskazini na magharibi mwa Iraq, ukiwemo mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Mosul.