Uganda yailalamikia DRC kwa vifo vya polisi wake

Image caption Afisa mkuu wa Polisi nchini Uganda Edward Kayihura

Serikali ya Uganda imewasilisha ombi rasmi kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya maafisa wanne wa Uganda kupigwa risasi katika Ziwa Albert,ambalo linagawanya mpaka wa mataifa hayo mawili kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Wanne hao waliuawa wakati walipokuwa wakichunguza uvuvi haramu unaotekelezwa katika ziwa hilo.

AFP ilimnukuu waziri wa maswala ya kigeni Henry Okello Oryem akisema kuwa maafisa hao wanne walikuwa kazini katika eneo la Uganda.

''Waliuawa wakiwa kazini na miili yao kuchukuliwa na mamlaka ya DRC.Tumeweka wazi,katika siku za usoni visa kama hivi vitaishinikiza Uganda kujilinda ikiwemo kuwatafuta wahusika''.