Ofisi za Google zavamiwa Ufaransa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ofisi za Google zavamiwa Ufaransa.

Maafisa wa kukusanya kodi nchini Ufaransa wamevamia makao makuu ya kampuni ya Marekani ya Google kama sehemu ya uchunguzi unaohusu ukwepaji kulipa kodi.

Ripoti zinasema kuwa karibu maafisa 100 wa kukusanya kodi waliingia ofisi za Google kati kati mwa Paris mapema asubuhi.

Google inadaiwa kima cha dola bilioni 1.7 na serikali ya ufaransa za kodi.