Islamic State yashambuliwa Syria na Iraq

Haki miliki ya picha Manbar.me

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu Islamic State linakabiliana na vikosi aina mbili tofauti vinavyojaribu kuliondoa kundi hilo katika maeneo yanahodhi nchini Syria na Iraq.Kundi la kikurdi la muungano wa makundi yaliyojihami kaskazini mashariki mwa syria limetangaza kuanza kwa kampeni karibu na himaya yake iliyopo katika mji wa Raqqa.

Muungano huo unakisiwa kupeleka wapiganaji elfu thelathini.Washington na Moscow zimethibitisha kuunga mkono.

Nchini Iraq, vikosi mbalimbali vya jeshi, na watu wa makabila ambayo yanaunga mkono serikali iliyopo madarakani wanaendelea kupambana na kundi la IS katika mji wa Falluja.