Marcus Rashford kupewa fursa dhidi ya Australia

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Marcus Rashford

Marcus Rashford huenda akaanzishwa katika timu ya soka ya Uingereza dhidi ya Australia siku ya Ijumaa,lakini meneja Roy Hodgson anasema kuwa ana wakati mdogo wa kuonyesha umahiri wake kabla ya michuano ya Euro 2016.

Kocha Hodgson anasema kuwa haogopi kumpatia fursa mchezaji huyo chipukizi na kuongezea kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ana kipawa.

Lakini akaongezea kuwa hakuna fursa nyingi kwa Rashford kuonyesha uwezo wake katika timu ya Uingereza.

Rashford alianza kuichezea klabu ya Manchester United mnamo mwezi Februari na amefunga mabao manane katika mechi 17.

Hodgson ana hadi Mei 31 kutaja kikosi chake cha watu 23 cha michuano ya Euro 2016,ambayo inaanza tarehe 10 mwezi Juni.