Waandamanaji wampinga Trump New Mexico

Trump Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji walitatiza hotuba ya Trump Albuquerque

Waandamanaji wanaompinga mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump wamekabiliana na polisi katika jimbo la New Mexico.

Walikuwa wakiandamana katika eneo ambapo Bw Trump alikuwa akifanya mkutano wake wa kampeni, nje ya ndani ukumbi mkuu wa mikutano wa Albuquerque.

Wamerusha fulana zilizokuwa zikiwaka moto zilizokuwa zimeandikwa kauli mbiu za kampeni ya Trump amoja na mawe an chupa za plastiki.

Polisi wa kukabiliana na fujo wametumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.