Kanali mstaafu wa jeshi auawa Burundi

Mauaji Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mauaji yamekuwa yakitekelezwa Burundi tangu ghasia kuzuka Aprili mwaka jana

Kanali mmoja wa kijeshi aliyestaafu ameuawa kwa kupigwa risasi huku mwanawe akijeruhiwa kwenye shambulizi la hivi punde katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.

Rufyiri Lucien alipigwa risazi alipokuwa ndani ya gari lake akisubiri kufunguliwa mlango katika mtaa wa Ngagara.

Alipigwa risasi kichwani huku mwanawe ambaye alikuwa akifungua mlango akipata majeraha madogo.

Kwingineko jana usiku, watu waliokuwa na silaha walimuua polisi na raia mmoja katika wilaya ya Ndava iliyo eneo la Mwaro nchini humo.

Taifa la Burundi limekumbwa na mauaji tangu rais Pierre Nkurunziza kuponea jaribio la mapinduizi na mandamano ya kumtaka aondoke madarakani baada ya kuongoza kwa miaka kumi.