Jeshi la Kenya laua wanamgambo 21 Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi la Kenya linasema liliwawinda wanamgambo hao baada ya msafara wao kushambuliwa magharibi mwa Somalia.

Jeshi la Kenya linasema kuwa limewaua wapiganaji 21 wa kundi la al-Shahab nchini Somalia.

Jeshi liliwawinda wanamgambo hao baada ya msafara wao kushambuliwa magharibi mwa Somalia, kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo.

Al-Shabab inasema kuwa wapiganaji wake waliwaua wanajeshi watano , wakawajeruhi wanne na kuchoma gari moja la kijeshi wakati wa mapigano hayo.

Jeshi la kenya halikusema ikiwa lilikumbwa na maafa yoyote.

Wanajeshi wa Kenya waliingia nchini Somalia mwaka 2011, kuwapiga vita wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.