Walemavu wapambana na serikali Bolivia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Bolivia Morales

Polisi nchini Bolivia wamepambana na waandamaji walemavu ambao walikuwa wakijaribu kwenda ikulu kudai nyongeza za mafao.Serikali ya Bolivia imesema polisi wamepambana na waandamaji hao kwa kutumia maji ya kuwasha mwilini walipovamiwa na kundi la waandamanaji ambao walijaribu kuvuka mpaka uliowekwa na kujaribu kuvamia polisi kwa kutumia visu.

Waandamanaji hao wameweka kambi katika uwanja wa La Paz kwa muda wa mwezi mmoja sasa.Waandamanaji hawa wamekasirika baada ya vurugu kutokea.

"haya ndio maisha tunayoishi. Tulichoomba ni kupewa hadhi kwa watu wenye ulemavu na hiki ndio rais wa Bolivia anachofanya. Hivi ndivyo anavyotaka, polisi kutupiga na kutudhalilisha."

Raia hao wanaoishi na ulemavu wanadai ongezeko la mafao yao ili kufikia angalau dola kumi na nne kwa mwezi.