Donald Trump
Huwezi kusikiliza tena

Donald Trump aungwa mkono na Republican

Donald Trump amesema amefurahishwa kuona kuwa amepata kuungwa mkono na wajumbe wa kutosha kutoka chama chake cha Republican hivyo kuweza kushinda uteuzi wa chama chake katika kinyang'anyiro cha urais wa nchi hiyo hapo mwezi July.

Trump alikuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya wakala wa habari Associate Press na NBC News kukisia kwamba hivi sasa Trump ana wajumbe zaidi ya elfu moja mia mbili na thelathini na saba - ambao wanatosha kumhakikishia amepata uteuzi wa chama chake.

Awali mwandishi wa BBC Regina Mziwanda alizungumza na Mubelwa Bandio ambae ni mkazi wa Silver Spring Maryland huko nchini Marekani na kumuuliza je wamarekani wameridhishwa ha hatua hiyo?