Maandamano ya kumpinga Kabila yafanyika DRC

Image caption Waandamana kumpinga kabila

Maandamano ya upinzani yanafanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia madarakani baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika maeneo mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa mgombea wa urais wa Upinzani Moise Katumbi.

Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.

Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.

Image caption Waandamana Kumpiga kabila

Mjini Goma katika eneo la Birere,amesema kuwa ni mchezo wa paka na panya ambapo vijana wamekuwa wakijibizana na polisi kwa kuwarushia mawe huku nao maafisa hao wakiwatupia vitoa machozi.

Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa polisi.