Mugabe asema kuwa haondoki madarakani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mugabe asema haondoki madarakani.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa yeye sio Mmarekani wala Muingereza wakati akiwahutubia karibu watu 50,000, wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika kwenye mji mkuu Harare kwa heshima yake.

Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amekana uwezekano wowote wa kuondoka madaraklani na kuwashambulia viongozi hasimu ndani ya chama tawala cha ZANU-PAFU kwa kupanga kumrithi.

Amesema kuwa yeye anawahudumia watu wa Zimbabwe na kuwa ataondoka tu ikiwa watu wangetaka afanye hivyo. Hata hivyo amesema kuwa haondoki na haendi popote.