Kampuni ya teksi ya Uber kuingia Tanzania na Uganda

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Teksi za Uber

Kampuni ya Teksi za Uber imesema kuwa itaanzisha huduma zake katika miji ya Ghana,Tanzania na Uganda katika kipindi cha mwezi mmoja kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Uber tayari imeanzisha huduma zake katika mataifa tisa ya jangwa la Sahara ikiwemo Nigeria,Afrika Kusini na Kenya.

Meneja mkuu wa kampuni hiyo Alon Lits wa eneo la jangwa la Sahara barani Afrika amesema kuwa kampuni hiyo pia inapanga kuanzisha mfumo wa kulipa pesla taslimu nchini Afrika Kusini,ikiongezea mfumo wake wa kielektroniki wa kufanyia malipo.

Biashara za Uber teksi ziliongezeka nchini Kenya ,ambapo watu wengi hawatumii kadi za kielektroniki kufanya malipo baada ya malipo ya pesa taslimu klkubalika.