Cantona amlaumu Deschamps kwa ubaguzi

Image caption Eric Cantona

Mwakili wa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amesema kuwa atamshtaki Eric Cantona kwa ksea kuwa kikosi chake cha Euro 2016 kilichaguliwa kwa ubaguzi.

Cantona alisema siku ya Alhamisi kwamba Deschamps aliwawacha kwa makusudi wachezaji wawili wenye miziz yao Afrika karim Benzema na Hatem ben Arfa nje ya kikosi hicho.

''Benzema ni mchezaji mzuri'', ''Ben Arfa pia ni mchezaji mzuri'',aliambia gazeti la the Guradian.Lakini Deschamps,ana jin la Kifaransa.

''Pengine ni yeye pekee nchini Ufaransa ambaye ana jina la Kifaransa''.Aliendelea kusema:''Ben Arfa pengine ndio mechezaji bora Ufaransa leo.lakini wana mizizi yao''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa kikosi cha Ufaransa

Ninarahusiwa kufikiria kuhusu hilo.

Akizungumza na gazetin la michezo L'Equipe,wakili wa Deschamps ameyataja matamshi hayo kama yasio kubalika ,ya kumuharibia jina na kwamba mteja waki atakwenda mahakamani.