Walioachiliwa huru Uganda wakamatwa tena

Suleiman Mbuthia
Image caption Suleiman Mbuthia ni mmoja wa waliatikana bila hatia

Washukiwa watano walioondolewa makosa ya kuhusika kwenye mashambulio ya mabomu ya mwaka 2010 mjini Kampala, Uganda wamekamatwa tena.

Mawakili wa watano hao wameambia wanahabari kwamba washukiwa hao wamekamatwa na kupelekwa nje ya Kampala.

Gazeti la serikali ya New Vision limeripoti kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ameambia mahakama watano hao walikamatwa kabla ya kufikishwa gereza la Luzira.

Hii ni baada ya wakili wa washtakiwa kulalamikia mahakama kwamba washukiwa waliokuwa wameachiliwa huru walikuwa wametoweka.

Waliopatikana bila hatia ni Abubakari Batemyetto, Omar Awadh Omar, Yahya Suleiman Mbuthia, Mohamed Hamid Suleiman na Dkt Ismael Kalule.