Uingereza kupeleka wanamaji wake Libya

Haki miliki ya picha EPA
Image caption David Cameron

Taifa la Uingereza linatarajiwa kutuma meli ya jeshi lake la wanamaji katika bahari ya Mediterenean ili kusaidia kuzuia kupenyezwa kwa silaha nchini Libya ,waziri mkuu David Cameron ametangaza.

Ameuambia mkutano wa G7 nchini Japan kwamba Uingereza iko tayari kuchukua uongozi katika kusaidia Libya kuzuia biashara ya ulanguzi wa watu na mgogoro wa uhamiaji.

Uingereza tayari ina meli ya HMS Enterprises inayopiga doria katika eneo hilo.

Maafisa wa meli hiyo wanasubiri amri ya Umoja wa Mataifa kwa meli hiyo ya kivita kukamata boti zinazosafirisha silaha kwa wapiganaji wa Islamic state.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Wanamaji wa Uingereza

Wiki iliopita,Serikali mpya ya National Accord GNA nchini Libya ilitaka Muungano wa Ulaya ulio na ujumbe wake unaoitwa Operesheni Sophia ,katika eneo hilo kwa usaidizi.

Imetaka usaidizi katika mafunzo ya wanamaji na walinzi wake wa pwani mbali na kuzuia ulanguzi wa watu katika bahari ya Mediterranean.