Wasio na ndugu China wapewa likizo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wazee China

Jimbo moja la Uchina, litawapa wafanyakazi wasiokuwa na ndugu, siku 21 za likizo kila mwaka, kusaidia kuangalia wazee wao wakongwe.

Uamuzi huo utasaidia kushughulikia matokeo yasiyotarajiwa, ya sera ya miaka mingi, ya kuruhusu watu kuwa na mtoto mmoja tu ambayo yamepelekea mamilioni ya familia, kuwa na mtoto mmoja tu kuangalia wazee wawili wakizeeka.

Jimbo la Henan, litatoa likizo hiyo zaidi, kwa wafanyakazi wenye wazee wanaopindukia umri wa miaka 60, na waliolazwa hospitali.

Mwaka jana, Uchina ilifuta sera hiyo ya mtoto mmoja, ili kurekibisha jamii ambayo inazeeka.