Uturuki yasema imewaua wapiganaji 100 wa IS

Haki miliki ya picha AFP getty Images
Image caption Wanajeshi wa Uturuki

Jeshi la Uturuki linasema kuwa mizinga yake imewaua wapiganaji zaidi ya mia moja wa IS nchini Syria.

Waturuki wanasema waliwalenga wapiganaji hao, ambao walikuwa wanakaribia kurusha makombora kushambulia Uturuki, upande wa pili wa mpaka, hapo jana.

Lakini haijulikani vipi jeshi la Uturuki, liliweza kuhisabi idadi hasa ya hasara iliyosababisha, katika eneo linalodhi-bitiwa na IS, na hakuna njia ya kuripoti kutoka eneo hilo.