Kampuni yaomba msamaha kwa tangazo la kibaguzi

Haki miliki ya picha QIAOBI

Kampuni moja ya matangazo ya sabuni ya kufua nguo, nchini China ambayo imesababisha ukosoaji mkubwa mitandaoni kwa matangazo yake ya kibaguzi, imeomba msamaha.

Kampuni hiyo iitwayo Qiaobi, inayotengeneza sabubi ya unga unga, imesema kuwa inapinga vikali ubaguzi wa aina yoyote.

Haki miliki ya picha Qiaobi

Katika majibu yake ya awali siku kadhaa zilizopita, kampuni hiyo ilisema kwamba, haikufikiria juu ya swala hilo la ubaguzi, huku ikishikilia kuwa wakosoaji wake wa mataifa ya kigeni wana lalamika bure.

Matangazo hayo ya kibiashara yanaonyesha mtu mweusi anaingizwa ndani ya mashine ya kufua nguo kabla ya kutokea akiwa na ngozi ya mtu mweupe, sawa na raia wa Bara Asia.