India yaahidi kuwalinda waafrika

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Wanafunzi wa afrika walalamikia kubaguliwa nchini India.

Serikali ya India imeahidi kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaowadhulumu na kuwadhalalisha raia wenye asili ya kiafrika, wanaoishi katika mji mkuu wa Delhi.

Katika wiki kadhaa zilizopita, kumeshuhudiwa dhulma dhidi ya waafrika mjini Delhi.

Waziri wa maswala ya ndani nchini humo, Rajnath Singh, amesema kuwa amewaamrisha polisi mjini Delhi kuwakamata washukiwa.

Image caption Kisa hicho kilisababisha malumbano makali kutoka kwa balozi kadha za mataifa ya Afrika na utawala wa India.

Visa sita dhidi ya waafrika tayari vimeripotiwa. Katika kisa kibaya zaidi,raia mmoja kutoka Congo alipigwa hadi kufa kufuatia vuta nikuvuta baada ya kukodi kjigari aina ya Tuk Tuk.

Kisa hicho kilisababisha malumbano makali kutoka kwa balozi kadha za mataifa ya Afrika na utawala wa India.