Mwanamke aliwa na Mamba Australia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mamba

Polisi kaskazini mwa Australia wanasema kuwa mwanamke mmoja hajulikani aliko, baada ya kushambuliwa na mamba alipokwenda kuongelea usiku.

Mwanamke huyo na rafiki yake walikuwa katika kidibwi chenye kina kifupi katika hifadhi ya kitaifa ya wanyama pori ya Daintree.

Hifadhi hiyo ya taifa ipo katika maeneo ya Queensland, nchini humo.

tukio hilo ni limetokea Jumapili jana, ambapo hadi sasa inahofiwa kuwa huenda ameliwa na Mamba.