Akamatwa kwa kuvaa fulana yenye picha ya Besigye

Image caption Polisi wanasema kuwa watu hao walikamatwa kwa sababu walikuwa wamepanga kufanya maandamano

Baadhi ya raia nchini nchini Uganda wamelaumu hatua ya kukamatwa kwa mwanamme moja ambaye anadaiwa kuvaa fulana yenye picha na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Samson Tumusiime alikamatwa mwishoni mwa wiki.

Hivi majuzi aliweka picha kwenye mtandao wa Facebook akiwa amevaa fulana hiyo.

Watu wengine wawili ambao wanadaiwa kuchapisha fulana hiyo nao wamekamatwa

Kulingana na msemaji polisi Fred Enanga, ni kuwa washukiwa hao watatu walikamatwa kwa sababu walikuwa wamepanga kufanya maandamano yaliyo kinyume na sheria.