IS na jeshi la serikali wapambana Fallujah

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption vikosi vya serikali dhidi ya IS Fallujah

Vikosi vya serikali nchini Iraq vinapambana na wapiganaji wa IS ili kuukomboa mji mji wa Fallujah unaoshikiliwa na wana mgambo hao.

Hata hivyo wanakabiliwa na upinzani mkali ili kuweza kusonga mbele.

Maofisa wa jeshi la serikali wamesema kuwa wanendesha mapambano hayo kwa uangalifu mkubwa kuhakikisha kuwa hawaleti madhara kwa raia.

Mamia ya watu wamekimbia makazi yao katika mji wa Fallujah na sasa wanaishi kwenye kambi zilizoko Barzinjah,kilomita 400 kaskazini mwa mji huo.

Baadhi ya raia katika mji huo wanasema mapigano hayo yamesababisha kujeruhiwa kwa familia zao.