Kenya: Wakimbizi Daadab kurejeshwa kwao Novemba

Haki miliki ya picha
Image caption Kambi ya Daadab kufungwa Novemba; Kenya

Kambi ya wakimbizi ya Daadab itafungwa kabla ya mwezi Novemba mwaka huu.

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya bwana Joseph Nkaisserry amekariri kauli ya serikali yake kuwa hakutakuwa na mazungumzo zaidi kuhusiana na hilo.

Hata hivyo waziri huyo ameiambia BBC kuwa serikali kwa ushirikiano na serikali ya Somalia na kitengo kinachoshughulikia maswala ya wakimbizi cha Umoja wa Mataifa itahakikisha uhamisho huo inafanyika kwa njia nzuri.

Kenya tayari imetenga takriban dola milioni kumi kufanikisha shughuli hiyo ambayo inasema kuwa inalenga kuihakikishia usalama wake kufuatia msururu wa mashambulizi ya kigaidi yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la al Shabaab.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kenya, inasema kuwa uhifadhi wao unaiathiri Kenya kiuchumi,usalama na kimazingira.

Waziri huyo aliyasema hayo katika hafla na wanahabari baada ya kupokezwa ripoti kuhusiana na kufungwa kwa kambi hiyo ya wakimbizi.

Kambi hiyo ambayo ndio makao ya takriban wakimbizi laki sita wengi wao kutoka Somalia imelaumiwa kuwa mwenyeji wa magaidi waliopanga na kufanikisha mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.

Kenya, inasema kuwa uhifadhi wao unaiathiri Kenya kiuchumi,usalama na kimazingira.