Waziri Mkuu wa Pakistan afanyiwa upasuaji wa moyo

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Waziri mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif, amefanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali moja jijini London Uingereza.

Waziri mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif, amefanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali moja jijini London Uingereza.

Bintiye Maryam, ametangaza hayo katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Amesema kuwa operesheni imekamilika vyema na kwa sasa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Bintiye Maryam, amesema kuwa operesheni imekamilika vyema na kwa sasa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

''Upasuaji umekamilika vyema''

''Mishipa yote sasa imepandikizwa na sasa anepelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi'' alisema Maryam katika mtandao wake wa Twitter

Aidha aliongezea kuwashukuru wale wote waliomuombea babake kabla na hata baada ya upasuaji huo.

''Natanguliza shukrani zote kwa wale wote waliomuombea babangu,mungu atawabariki nyote''

Bwana Sharif, mwenye umri wa miaka 66 anatarajiwa kusalia hospitalini kwa zaidi ya wiki moja kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Anaaminika kuwa mojawepo wa watu tajiri zaidi nchini Pakistan.

Afisa mmoja wa serikali ya Pakistan amesema kuwa waziri huyo mkuu amejilipia fedha zote za upasuaji.