Jaribio la kombora la Korea Kaskazini lafeli

Haki miliki ya picha AP
Image caption Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imefanya jaribio jengine la makombora yake ya masafa marefu katika eneo la mashariki ya pwani yake lakini linaonekana kufeli,wanajeshi wa taifa hilo wamesema.

Haijulikani ni kombora gani ,lakini linajiri baada ya makombora mengine kwa jina ''Musudan'' kufeli mnamo mwezi Aprili.

Korea Kaskazini imepigwa marufuku na Umoja wa Mataifa kutumia teknolojia yoyote ya makombora ya masafa marefu.

Wasiwasi umetanda katika eneo hilo baada ya Pyongyang kujaribu kombora la nne la Kinyukia mnamo mwezi Januari pamoja na makombora mengine.