Kampuni ya ndege kusitisha safari

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bendera ya Venezuela

Kampuni kubwa ya ndege ya Latini America,iitwayo Latam,imesema kuwa itasitisha huduma zake za usafiri nchini Venezuela kutokana na kudorora kwa uchumi wa nchi hiyo.

Zuio hilo linakuja siku moja baada ya shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa kusema litazuia safari zake kwenda nchini humo mwezi ujao, kutokana na nchi hiyo kuwa na mzigo wa madeni katika mapato ya tiketi.

Venezuela yenye utajiri wa mafuta imeathirika zaidi na kushuka kwa bei ya mafuta duniani,inakabiliwa na mfumuko wa bei na uhaba wa bidhaa muhimu.

Mashirika kadhaa ya ndege yamesema kuwa kutokana na uchumi wa nchi hiyo kudorora inakuwa ngumu kupata fedha za kigeni kama dola kwa ajili ya kubadilisha kimataifa.

Juma lililopita kampuni ya Coca Cola pia ilitangaza kusimamisha baadhi ya huduma zake kutokana na kukokosekana kwa sukari.