Walioambukizwa Zika kutumia kondomu

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mtoto aliye na virusi vya Zika

Shirika la Afrika Dunia (WHO) sasa linawahimiza watu wanaotoka katika sehemu zilizoathirika na virusi vya Zika kuzingatia mbinu za kujikinga endapo mtu anafanya mapenzi ama kujiepusha na ngono kwa muda wa wiki nane.

WHO pia imeongeza kwamba wanawake waepukane na kupata mimba kwa miezi sita iwapo mwenzake wa ndoa amekuwa na dalili za virusi vya ugonjwa huo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Zika

Wiki iliyopita shirika hilo lilisema hakuna sababu ya kujiepusha na michezo ya Olimpiki mjini Rio mwezi Agosti.

Hii inaongezea vigezo vya hapo awali .