WHO: Pakiti za sigara kukosa maandishi

Image caption WHO: Pakiti za sigara kukosa maandishi

Mpango wa upakiaji wa sigara katika pakiti zisizokuwa na maandishi utaenezwa kote duniani, katika hatua itakayobadilisha kwa kiasi kikubwa hali ya afya duniani.

Shirika la afya duniani,WHO limetangaza mpango huo utakao anza kwa mabadiliko ya sera katika mataifa ya Uingereza, Ufaransa na Australia.

Kauli hiyo hata hivyo imepingwa vikali na muungano wa kampuni zinazotengeneza sigara duniani ikisema kuwa kamwe kauli hiyo haina msingi wowote.

Kila mwaka takriban watu milioni 6 hufaa kutokana na maambukizi yanayohusishwa na uvutaji sigara.

Upakiaji wa sigara katika mapakiti yasiyokuwa na maandishi yeyote ila yale ya kutahadhari watu dhidi ya uvutaji sigara yamepigiwa upatu kupunguza hamu ya kuwavutia wateja wapya wa kuvuta sigara.

Kulingana na mpango huo wa WHO mapakiti hayo yatakuwa na nembo zisizovutia na zenye rangi moja.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Kulingana na mpango huo wa WHO mapakiti hayo yatakuwa na nembo zisizovutia na zenye rangi moja.

Kauli hiyo inatokana na utafiti kuwa mabadiliko hayo yatawanyima raha wavutaji sigara kwa mujibu wa afisa wa WHO Benn McGrady.

Tangu Australia ilipoweka sheria hii mwaka wa 2012 uvutaji sigara ulipungua kwa asili mia 0.55% ambayo ni sawa na takriban watu 108,000 kati ya mwezi Desemba 2012 na Septemba 2015 taarifa hiyo ya WHO inaelezea.

Bw McGrady aliiambia BBC kuwa , ''Bila shaka kuna upinzani kutoka kwa makampuni yanayotengeneza sigara ila tukizingatia ushahidi kutoka Australia tunaona kuwa hii ndio njia mwafaka ya kupigana na uvutaji sigara duniani''

''Mataifa yote yanapaswa kuiga mfano huo wa Australia ilikufuta uvutaji sigara''

Mataifa mengine yanayoonesha hamu ya kuiga mfano huo ni - Ireland, Norway, Singapore, Canada, Chile, Brazil, Panama, New Zealand na Ubelgiji .