Shambulio la al-shabab hotelini lawaua watu 10

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulio la al-Shaba hotelini

Wapiganaji wamevamia hoteli moja katikati mwa mji wa Somalia Mogadishu huku kukiwa na ripoti kwamba huenda takriban watu kumi wameuawa.

Wanadaiwa kuingia katika Hoteli ya Ambassador katika barabara ya Maka al-Mukarama baada ya kulipua bomu lililotegwa ndani ya gari,ripoti zimesema.

Kundi la wapiganaji wa al-Shabab limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Mwandishi wa BBC katika idhaa ya Somali amesema kuwa mlipuko huo ni miongoni mwa milipuko mikubwa kukumba mji huo na uharibifu wake ni mkubwa zaidi.