Adele amkomesha aliyekuwa akimrekodi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Adele amkomesha aliyekuwa akimrekodi

Mashabiki wa mwanamuziki nyota wa Rock Adele walipigwa na butwaa msanii huyo wa kizazi kipya aliposimamisha 'shoo' yake katikati ilikuwapa muda maafisa wa usalama kumzuia shabiki mmoja aliyekuwa akirekodi video ya shoo hiyo.

Adele ambaye aligonga vichwa vya habari duniani kwa kuuza albamu nyingi zaidi mwaka uliopita alikonga nyoyo za mashabiki kote duniani kwa kibao chake cha Hello.

Hata hivyo hapo jana Adele hakutaka mzaha na hati miliki.

Alipomuona mwanamke huyo akirekodi video, Adele ambaye alikuwa jukwaani akiwatumbuiza mamia ya mashabiki waliokuwa katika ukumbi huo wa Verona nchini Italia, alisitisha wimbo huo na aakamsihi aache.

''tafadhali mbona unanirekodi ,mbona usiketi chini na usikize burudani moja kwa moja, mimi niko hapa nawe mbona unanirekodi ?alifoka mwanamuziki huyo raia wa Uingereza.

''Hii sio DVD hii ni moja kwa moja na wewe kuendelea na kunirekodi kunawasumbua wale waliolipia kuja hapa kujiburudisha''.

''Unafahamu kuwa watu wengi wameshindwa hata kuingia hapa kwa hivyo ingekuwa bora zaidi iwapo ungefunganya madude hayo uketi chini raha mstarehe uburudike pasi na kuwazuia mashabiki wenzako''.