Mashirika ya kimataifa yaonywa Sudan

Image caption Ndege ya Umoja wa Mataifa

Jeshi la Sudan limeshtumu mashirika ya kigeni kwa kukiuka anga yake na limeonya kwamba litakabiliana nayo vilivyo,kulinga na chombo cha habari cha AFP.

Ndege ya mizigo inayofanyia kazi mashirika ya kimataifa na yale ya kieneo ilikiuka anga ya Sudan manmao tarehe 17 na 20 mwezi Mei ,kulingana na taarifa ya AFP.

Jeshi la Sudan limeonya kwamba ndege yoyote inayokiuka anga ya taifa hilo na kuingia bila ruhusa ama maelezo itakabiliwa vilivyo,alisema msemaji Brigadier Ahmed Khalifa al-Shami.

Jeshi hatahivyo halikutaja jina la shirika hilo.Jeshi la Umoja wa mataifa katika eneo la Darfur na shirika la chakula duniani hufanya operesheni zake kila siku kupitia Sudan.

Wikendi iliopita serikali ilimfurusha kiongozi wa Umoja wa Mataifa anayesimamia misaada ,hatua iliokosolewa na kiongozi wa Marekani katika Umoja huo.